June 11, 2013 at 4:36pm
Dunia kakuendea mrama
Maisha yakakusakama
Ndoto sasa zageuka njama.
Mwanamke huyo mwite 'Karma'
Mapenzi duni njo tizama
Yanaja bila shamrashamra
Yanakuchapa kwayo njora
Kukimbia utaona bora
Sifa zako zinadorora
Dunia duara ni onyo,
Wala si msemo wa mivinyo
Utakoma ja mtoto nyonyo
Sasa wajaliwa na sadfa
Mienendo yako ya kashfa
Na jina lako umechafya,
Majuto yako ya kugofya
Dunia kakuendea mrama
Maisha yakakusakama
Ndoto sasa zageuka njama.
Mwanamke huyo mwite 'Karma'
©davyvivaldi 2013
No comments:
Post a Comment