Monday, 3 June 2013

KIPENZI

Kipenzi
Nipashe yaliyo moyoni,
Niyafahamu jamani,
Ndani yangu pate amani
Vitendo vyangu vikupe imani
Kipenzi ni semeze jamani
Nipoze moto iliyorohoni
Kimya chako cha tatanisha
Kwa kweli wanibabaisha
lengo langu kufurahisha
Tabasamu lako kusadikisha
Kipenzi nasihi elimisha
mie nipate yako nasiha
Kipenzi ah!
Wanipa mi donda sugu
Moyoni wasababisha vurugu
Kimya chako tu, rohoni vuguvugu
Hata ni semeze kama ndugu
Angalau ondoa hii hofu
 

No comments:

Post a Comment

Featured post

DID I?

Did I tell you How lovely you are? The glimmer In the smile you have, The shine it gives To this colourful world Did I tell you, Yo...