Monday, 3 June 2013

NGURUWE

Suti zako za madola, gari aina ya Bima,
Mlo wako sembuse mola, bili ya lisha nchi nzima,
Nyumba kubwa kule hola, waishi bila kupima
Wewe nguruwe ni mshindi, miungu kakupa pepo
...
Tumbo lako ndilo haja, wajibuwo kawa ovyo
Mifuko kwako ndyo haja, roho wako wa uchoyo
Mkono birika wa taja, utu katoweka moyo
Wewe nguruwe ni mshindi, miungu kakupa pepo.
 
 Heshima ndio wataka, eti mtumishi wa watu
Haki zetu wazibaka, na mawazo yenye kutu,
Akilio mejaa taka, heri tusihi majitu
Wewe nguruwe ni mshindi, miungu kakupa pepo

Hauna hata adabu, katiba ka kojolea
unatupea aibu, kwenye pipa wa bobea
Hulka zako za ajabu, mifukoyo kuombea
wewe nguruwe ni mshindi, miungu kakupa pepo.

No comments:

Post a Comment

Featured post

DID I?

Did I tell you How lovely you are? The glimmer In the smile you have, The shine it gives To this colourful world Did I tell you, Yo...